Wema Isaack Sepetu huenda akawa ndiye staa ambaye kwa historia ya Bongo, mwenye matukio ya kusikitisha zaidi.
Ingawa utafiti rasmi haujafanyika lakini ni wazi, kwa matukio yanayowahusu mastaa wa Bongo hususani yale yenye kusikitisha na kufedhehesha, binti Sepetu anaweza kuwa kinara.
Ingawa ni mengi na si vyema kuyakurupusha yalikopumzika lakini hili la kukamatwa na vidhibiti vya matumizi ya dawa za kulevya, limekuja na ‘msaidizi wake’.
Baada ya kuingia kwenye mikono ya Makonda kwa kesi ya dawa za kulevya kisha kutolewa kwa dhamana staa huyo alitarajia kufarijiwa na mashabiki pamoja na watu wengine wenye moyo wa kibinadamu.
Kinyume chake, mwanasheria aliyemsaidia, Albert Msando ametoa ushuhuda na kudai kuna watu ‘wanamlaumu’ kwanini amemsaidia Wema?
Wema anachukiwa uraiani? Kuna watu wanatamani Wema apotelee gerezani?
Jawabu lake amelitoa Msando kupitia maneno yake aliyoyaweka Instagram:
‘Kuna watu wameongea walichoongea. Wamekasirika kumsaidia Wema,’.
‘Ila ukweli unabaki kwamba Wemasepetu has her following. I must say yeye kama ilivyo mimi na wewe sio mkamilifu. She has her share of mistakes. And failures. But she is not a bad person. She has a special heart.
Kwa hiyo kwa wale ambao wameamua kupigana vita kwa kuniattack I am leaving it to them. For me all I have to do is, guide her to being better and realising her full potential. Thats not law. Thats friendship’.
Umechukia Wema Sepetu kutoka rumande? Basi jawabu kwa waliochukia na kumshambulia mwanasheria huyo ni