Mkuu wa mkoa wa Mjini Magharibi visiwani Zanzibar, Ayoub Mohamed Mahamoud amesema kuwa baa zitafanya kazi masaa manne tu ndani ya siku kuanzia saa kumi jioni hadi saa mbili usiku.
Kauli ya mkuu wa mkoa huyo inakuja baada ya kukithiri kwa vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia na ongezeko la wimbi la madada poa visiwani humo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati za Baa Zanzibar, Hussein Ali Kimti amesema kitendo cha kupunguza muda wa saa za kazi kutapelekea ugumu mkubwa wa maisha yao ya kila siku kwani ni wazi kipato chao kitaporomoka kwa kasi kubwa kutokana uchache wa muda.
Naye Mwanasheria wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Vyakula na vinywaji Zanzibar, Hassan Cornel amesema agizo lililotolewa na mkuu huyo wa mkoa ni zito kwa wafanyabiasahra hao kwani wamekuwa wakilipa kodi hivyo amemtaka kuweka mikakati mizuri ili kuendana na mazingira ya kodi zao.