Aliyekuwa mshambuliaji wa Azam FC, Kipre Tchetche amekshindwa kuichezea klaby yake mpya ya Al-Nahda Al-Buraimi ya Oman kutokana na klabu hiyo kushindwa kumalizana na Azam FC.
Kipre Tchetche amerejea nyumbani kwao Ivory Coast, baada ya Al-Nahda kushindwa kuwapa Azam FC dola za Kimarekani 50,000 (zaidi ya Sh. Milioni 100) walizotaka kumuachia mpachika nabao huyo.
Kipre Tchetche alikuwa amebakiza mwaka mmoja katika Mkataba wake Azam FC na akaondoka bila ridhaa ya klabu yake hiyo baada ya kuichezea kwa miaka mitano.
kipre Tchetche alijiunga na klabu hiyo ya Oman kwaajili ya msimu mpya wa ligi ya nchi hiyo.