Mwanamuziki wa mkongwe wa Bongo Fleva, AY amesema wakati anaenda kwenye tuzo za MTV alikuwa anabeba nyimbo za wasanii wengine kwa ajili ya kupata nafasi ya kupenya huko.
Pia amesema wasanii wa sasa wawe na upendo kwani hawezi jua kesho atakuwa wapi na atasaidiwa na nani.
“Zamani ulikuwa unapambana peke yako, mimi niliona sio sawa kusafiri peke yangu nikawa nabeba nyimbo za wasanii wenzangu kuwapelekea MTV, swali langu hawa wa sasa hivi wanaweza kufanya hivyo, nilikuwa nachukua hadi nyimbo za Kenya ili kupigwa MTV”
“Dawa ni kusambaza upendo tu, lazima tupendane haya maisha yapo tu, leo unaweza ukamfanyia mtu hivi kesho unamkuta yeye ndio boss you never know, video ya habari ndio hiyo au ngoja ageuke tulichukua mastaa kibao, hiyo ndio love”
“Napenda kuishi nikiwa Neutral sifungamani na chochote, Memory ambayo nikisema nimebugi sikumbuki japo nilikuwa napigwa vita ya chinichini, kwenye maisha hatuwezi kufanana kuanzia kwenye mpira, muziki au hata kwa madaktari” ameongeza