Mwanamuziki mkongwe wa Bongo Fleva, Ambwene Yessaya ‘AY’ amemvisha pete ya uchumba mpenzi wake anayefahamika kwa jina la Remy.

 Tukio la kumvalisha pete limefanyika jana siku ya Alhamisi na kuhudhuriwa na watu wake wa karibu akiwemo producer maarufu nchini kutokea B-Hits, Hami B.

Mwanamke huyo ambaye ni raia wa Rwanda alianza mahusiano na AY toka mwaka 2008 lakini jana wameamua kuweka wazi mahusiano yao.

AY alimtambulisha mpenzi wake huyo Disemba mwaka jana wakati wa birthday ya mrembo huyo.

Sherehe hiyo ilihudhuriwa na watu wa karibu na wawili hao, kwa kitendo hicho AY anatarajia kufuata nyayo za mwanamuziki mwenzake Profesa Jay ambaye amefunga ndoa wiki iliyopita.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *