Rais wa Klabu ya Simba, Evans Aveva na Makamu mwenyeki wa klabu hiyo Geofrey Nyange ‘Kaburu’ leo wamepandishwa kizimbani katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiwa na kesi ya utakatishaji fedha.

Baada ya kesi hiyo kusikilizwa viongozi hao wameshindwa kupata dhamana kutokana na makosa yao hivyo wamerudishwa rumande.

Aveva na mwenzake wamerudishwa rumande hadi Julai 20 mwaka huu kesi yao itakapotajwa tena katika mahakama hiyo.

Hhatua hiyo imetolewa leo na Hakimu Mkazi Kisutu, Victoria Nongwa wakati wa kusikilizwa kesi hiyo.

Kwa mujibu wa kesi inayowakabili viongozi hao wana mashtaka matano ambapo mawili kati ya hayo ni ya kutakatisha fedha, wamekosa dhamani kwa kesi yao ya utakatishaji fedha.

Viongozi hao walikamatwa na Takukuru mwezi uliopita wakikabiliwa na mashitaka ya kutakatisha fedha mpaka kupelekea kunyimwa dhamana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *