Kesi inayowakabili viongozi wa Simba, Evans Aveva na Geofrey Nyange ‘Kaburu’ imehairishwa mpaka Oktoba 11 mwaka kutokana na upelelezi kutokamilika.
Mwendesha Mashtaka wa TAKUKURU, Leornad Swai amemueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Godfrey Mwambapa kuwa shauri hilo limeitishwa kwa ajili ya kutajwa na upelelezi haujakamilika.
Kutoakana na hayo mwendesha mashtaki ameomba ipangiwe tarehe nyingine ambapo baada ya kueleza hayo Hakimu Mwambapa aliahirisha kesi hiyo hadi October 11, 2017.
Evans Aveva na Makamu wake, Geofrey wanakabiliwa na mashtaka matano ya kughushi, kuwasilisha nyaraka ya uongo na kutakatisha Dola za kimarekani 300,000.
Washtakiwa wapo rumande kwa sababu shtaka la kutakatisha fedha linalowakabili halina dhamana kabisa.