Rais wa Klabu ya Simba, Evans Aveva amelazwa katika kitengo cha wagonjwa mahututi Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Hayo yameelezwa leo Machi 8 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri na wakili anayewatetea, Evodius Mtawala wakati kesi hiyo ilipotajwa mahakamani hapo.

Hata hivyo, mwendesha mashtaka wa Takukuru, Leonard Swai naye ameliambia mahakama kuwa Aveva ni mgonjwa na kwamba upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.

Baada ya kutolewa kwa maelezo hayo, Mtawala ameiambia mahakama kuwa walizungumza na upande wa mashtaka wataeleza jalada la kesi hiyo bado lipo kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) na wameomba wapewe siku 14 ili waweze kueleza kitu.

Washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka matano ya  uhujumu uchumi ikiwamo kughushi, kuwasilisha nyaraka ya uongo na kutakatisha wa kiasi hicho cha fedha.

Hakimu Mashauri ameiahirisha kesi hiyo hadi Machi 22 mwaka huu itakaposikilizwa tena mahakamani hapo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *