Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli ametoa msaada wa vitanda, magodoro na mashuka katika hospitali ya Levolos iliyopo mkoani Arusha.

Msaada huo umekabidhiwa na mbunge wa viti maalumu wa CCM mkoa Arusha, Catherine Magige kwa niaba ya Rais Magufuli leo mkoani humo.

Mbunge amesema ametoa vitanda 25 ,mashuka 25 na magodoro 25 viliyotolewa na Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania ikiwa ni moja ya utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi

Pia amesema k uwa  kumekuwa na baadhi ya viongozi wamekuwa wakiponda kazi  za Rais na kusema kuwa  afanyikitu chochote

Aidha alitoa wito kwa wananchi kuunga mkono kazi ziazofanywa na Rais  ,pia alitumia muda huho kuwasihi madaktari kutunza vifaa ambavyo vinatolewa na serikali kwani vifaa hivyo vinanunuliwa kwa kodi za wananchi ,huku akisisitiza iwapo vitatunzwa vizuri vinaweza kukaa kwa muda mrefu na kuwahudumia wananchi wengi zaidi.

Akitoa shukrani kwa vifaa hivyo mkurugenzi wa jiji la Arusha, Athuman Kihamia aliishukuru serikali kwa kutoa misaada hii kwa jiji la Arusha na kuhaidi kuvitunza vifaa hivyo vilivyotolewa  huku akiiomba serikali iendelee kuwapa misaada ya aina mbalimbali.

Msaada huu wa magodoro 25 ,mashuka 25 pamoja na vitanda 25  uliogaiwa leo katika hospitali ya Levolosi jijini Arusha umetolewa na Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania  ikiwani moja ya utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *