Wasanii wa Bongo Fleva, Aslay na Nandy wamefunguka sababu ya kuachia wimbo wao mpya unakwenda kwa jina Subral kheri mpenzi uliotoka jana.
Wimbo huo wameurudi baadhi ya maneno kwenye wimbo ulioimbwa na aiyekuwa muimbaji wa taarab nchini marehemu, Nasma Khamisi Kidogo.
Aslay amesema kuwa alipokuwa Ya Moto Band alikuwa chini ya watu hivyo ilikuwa rahisi kusema anataka kufanyiwa sehemu yoyote video lakini sasa hivi anafanya mwenyewe ndio maana ameamua kurudi kule uswahilini ambapo yeye mwenyewe ametokea.
Kwa upande wa Nandy amesema kuwa wanawashakuru mashabiki wao kuupokea wimbo huo vizuri kinyume na matarajio yao na unaendelea ufanya vizuri.
Pia Nandy amefunguka tofauti zake na Ruby baada ya kusema watu wamekuwa wakiongea vitu vya uongo kuhusu wao lakini ukweli ni kwamba wao wako vizuri na kwa sababu wote wanafanya kazi sehemu moja ni vigumu sana kugombana.
Nandy ameongeza kwa kusema kuwa wanaweza kutoa wimbo na Ruby siku yoyote ile kwa sababu wote ni watoto wa nyumba moja, na kitendo cha kuwafananisha au kuwagombanisha sio kitu kizuri na hakiwezekani. hivyo watu wasikae wakitangaza na kuzusha vitu ambavyo havina ukweli.
Aslay na Nandy waliwahi kutoa wimbo uliokwenda kwa jina la Mahabuba ambao pia ulitamba kabla ya kuachia wimbo huu mpya.