Wanamuziki wa Bongo Fleva, Aslay na Nandy wanatarajiwa kuburuzwa Mahakamani kutokana na kuimba wimbo ‘Subalkher Mpenzi’ bila ya ridhaa ya wahusika.

Hayo yameibuka baada ya wamiliki wa wimbo huo, Kikundi cha Tarab Asilia visiwani Zanzibar (Culture Music  Club) kudai pesa zilizotolewa jumla ya Tsh. 800,000 kama fidia za kutumia kazi hiyo hawazitambui hivyo wanajipanga kuwapeleka mbele ya Mahakama.

Akizungumza Katibu Mtendaji wa kikundi hicho, Taimur Rukuni Twaha, amesema wasanii hao kabla ya kuimba tena upya wimbo huo walipaswa kuonana na uongozi huo ili kukubaliana jambo ambalo hawakufanya hivyo.

Kwa upande mwingine, Twaha amesema msimamo wao utabaki pale pale wa kuwafikisha Mahakamani wasanii hao endapo watashindwa kutimiza masharti waliyopewa na uongozi wa kikundi hicho.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *