Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Aslay Isihaka amesema kuwa amesikitishwa na kitendo cha kuzushiwa kifo wakati yupo hai na anaendelea na majukumu kama kawaida.

Kutokana na kutangaziwa kifo katika mitadaoni mwanamuziki huyo ameitaka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA, kuvichukulia hatua baadhi ya vyombo vya habari vya mitandaoni “Online Media” baada ya kumzushia kwamba amefariki dunia.

Kupitia akaunti yake Instagram Aslay ameandika kuwa “Inasikitisha na kushangaza sana unawezaje kumzushia mwanadamu mwenzako kifo na mabaya mengi, wanaofanya hivi ni Watanzania wa kawaida kama sisi ambao tulitamani watupe habari na burudani na wao wapate riziki, lakini wako bize kutupotosha na hata kuharibu majina yetu’.

Pia ameongeza kwa kuandika “Nawaomba sana TCRA wasiache kuzichukulia hatua online Tv makanjanja wengine wanaopotosha umma, tuna imani nanyi TCRA na Jeshi la Polisi na mamlaka nyingine, watu kama hawa wakiachwa, wanachafua taswira nzuri ya vyombo vingine vinavyofanya kazi kwa weledi.

Mwisho amemalizia kuandika kuwa “naheshimu sana waandishi wote bila kujali ukubwa wa vyombo vyao, lakini hawa makanjanja wachukuliwe hatua na kutokomezwa kabisa”.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *