Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Aslay amekanusha kuondoka na daftari la nyimbo za Yamoto Band baada ya kundi hilo kusambaratika na kila mmoja kufanya kazi kivyake.
Habari hizo za Aslay zilisambaa katika mitandao ya kijamii na vyombo vya habari kuwa ameondoka na daftari la Yamoto Band baada ya kuachia nyimbo kila kukicha ambapo hadi sasa hivi yeye ndiyo anaongoza kuachia nyimbo kuliko wasanii wenzake wa kundi hilo.
Aslay alikuwa mmoja kati ya wasanii waliounda kundi hilo ambalo lilivuma kwa miaka mingi na baada ya kuvunjika ambapo kwasasa kila mmoja anafanya kazi peke yake.
Kundi hilo lilisambaratika kutokana na masuala ya maslahi yaani uongozi wao ulikuwa hauwapi walichokuwa wanastahili na kusababisha kundi hilo kuvunjika.
Baada ya kuona kuwa katika muda mfupi ambao Aslay amekuwa peke yake amekuwa akitoa nyimbo nyingi kiasi like ndipo tetesi zilanza kusambaa kuwa Aslay aliiba daftari la nyimbo la Yamoto band lililokuwa na by nyimbo zilizo andikwa na wasanii wotenwakundi hilo.
Aslay tangu ameondoka katika kundi la Yamoto Band hadi sasa hivi ametoa nyimbo kama kumi na sita.