Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Aslay amesema kuwa kundi la Mkubwa na Wanawe halitoi sapoti kwa msanii anayefanya kazi binafsi.
Aslay ambaye anawakilihsa kundi la Yamoto Band amema hayo baada ya kuanza kufanya kazi binafsi bila kundi lake ambapo ameachia vibao kama viwili akiwa peke yake.
Mwanamuziki huyo amesema kuwa Mkubwa Fella anasimamia kundi zima la Yamoto Band lakini si kwa mwanamuziki mmoja mmoja kwa hiyo unatakiwa kufanya jitihada binafsi ili kuhakikisha muziki wako unafika mbali bila sapoti ya Mkubwa na Wanawe.
“Ni kweli Mkubwa yeye anasimamia Yamoto Band, Mkubwa hasimamii msanii mmoja mmoja, kwahiyo unatakiwa ufanye kitu cha ziada ilimradi ngoma zako zifike. Wenzangu wanaandaa vitu vinakuja lakini mimi nimefanya kama nimewahi kuwaonesha njia,”.
Kwa sasa Aslay ameachia wimbo wake mpya ‘Usiitie Doa’, aliomshirikisha malkia wa muziki wa taarab nchini Khadija Kopa ambao unafanya vizuri katika vituo mbali mbali vya Radio nchini.