Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Aslay amefunguka na kusema kuwa katika maisha yake ya mahusiano hajawahi kulizwa na mwanamke kisa mahusiano hivyo mapenzi.
Kauli ya mwanamuziki huyo inakuja kufuatia mashabiki kudai kuwa Aslay aliwahi kulia baada ya kuachana na aliyekuwa mpenzi wake ambae ni mzazi mwenzake Tesu Chocolate.
Msanii huyo amesema kuwa japokuwa alikuwa kwenye mahusiano na baadhi ya wanawake wengi nchini lakini hakuwahi kulia kwa ajili ya mapenzi kwasasa alikuwa anajua matatizo ya wanawake.
Aslay ambae alikuwa na mahusiano na mwanadada Tessy Chocolate kwa muda mrefu sana na kubahatika kupata mtoto mmoja lakini walikuja kuachana siku za baadae.
Mwanamuziki huyo kwasasa ametangaza kuwa hayupo kwenye mahusiano na mwanamke yoyote baada ya kuachana na mzazi mwenzake huyo.