Askari wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (Ecowas) wamegundua kemikali ya sumu kali iliyokuwa imetegwa kwenye vyumba vya Ikulu ya Gambia.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na Ecowas kupitia gazeti la Freedom la Gambia, kemikali hiyo ilitegwa kwa lengo la kuua mtu yeyote atakayeingia ndani ya Ikulu hiyo.

Kutokana na hali hiyo, kiongozi mpya wa Gambia, Adama Barrow,  anatakiwa kuendelea kukaa Senegal kwa usalama wake huku uchunguzi ukiendelea kufanyika.

Hayo yanajiri siku kadhaa baada ya aliyekuwa kiongozi wa nchi hiyo Yahya Jammeh kuondoka nchini humo na kuelekea Guinea uhamishoni baada ya kuachia madaraka.

Rais mpya wa nchi hiyo Adam Barrow yupo nchini Senegal alipopewa hifadhi ya muda kabla ya Yahya Jammen kuondoka ambapo anadaiwa kuondoka na zaidi ya dola milioni11 za Marekani kwenye hazina na Gambia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *