Jumla ya askari 14 wa Jeshi la Polisi Zanzibar wanatuhumiwa kushirikiana na waingizaji wa dawa za kulevya visiwani humo.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Ayoub Mohamed Mahmoud, mbele ya mbele ya Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia Dawa za Kulevya, Rogers Siyanga jana visiwani hum.

Mkuu wa mkoa huyo amesema hivi sasa wameshakamilisha utaratibu wa kuwafikisha askari hao katika vyombo vya sheria.

Amesema hatua hiyo inatokana na agizo lililotolewa na Rais Dk. John Magufuli, la kupiga vita uingizaji na utumiaji wa dawa za kulevya nchini.

Pia amesema hivi karibuni watu wanaofanya biashara hiyo kwa kushirikiana na watumishi wa Serikali ambao si waaminifu, walimuua mbwa aliyekuwa akifanya ukaguzi katika mizigo Uwanja wa Ndege.

Kwa upande wake Kamishna Siyanga amesema kuwa suala la mapambano dhidi ya dawa za kulevya si vita ya Dar es Salaam pekee ila ni ya Tanzania nzima, ikiwamo Zanzibar.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *