Mkurugenzi na mmliki wa bendi ya Twanga Pepeta, Asha Baraka amesema kuwa vyombo vya habari nchini vimechangia kuushusha muziki wa dansi.
Kauli hiyo inakuja baada ya muziki wa dansi kutofanya vizuri kwasasa kulinganishwa na hapo awali mpaka kupelekea muziki huo kukosa mvuto kabisa huku wapenzi wengi wakijikita kwenye muziki wa Bongo fleva.
Asha Baraka amesema kuwa vyombo vya habari Tanzania vimeshindwa kutotoa nafasi ya kutosha kuusapoti muziki wa dansi mpaka kupelekea muziki huo kupotea.
Pia Asha Baraka amesema miongoni mwa mambo mengine yanayokwamisha muziki wa dansi ni pamoja na wanamuziki wa dansi kuwa wakilazimishwa kufanya muziki bongo fleva.
Mkurugenzi amewataka wasanii wa dansi waanze kufanya nyimbo nzuri kama zamani, maana kwa sasa wamekata tamaa hivyo hawafanyi kazi nzuri kulinganishwa na hapo awali.
Asha ameongeza kwa kusema kuwa anaamini wizara yenye dhamana na maswala ya burudani itafanya juhudi za kusaidia kuurudisha muziki wa dansi katika chati kwa mwaka 2017.
Muziki wa dansi ni muziki uliojizolea umaarufu mkubwa miaka ya nyuma kutokana na nyimbo kupendwa na mashabiki wao kulinganishwa na hali ilivyo sasa.