Timu ya taifa ya Argentina imeendelea kushika nafasi ya kwanza kwenye orodha ya timu bora duniani.

Orodha hiyo imetolewa na Shirikisho la soka duniani (FIFA) hapo jana kwa nchi Wanachama wa shirikisho hilo.

Tano Bora kwenye orodha hiyo zimebaki zile zile bila mabadiliko na nazo ni Argentina (1), Brazil (2), Germany (3), Chile (4) na Belgium (5).

Misir wamekamata nafasi ya 23 baada kupanda Nafasi 12 wakifuata Senegal walio Nafasi ya 31 na Mabingwa Wapya wa Afrika ambao ni Cameroon, wapo Nafasi ya 33 baada kupaa Nafasi 29 huku Tanzania ikishuka Nafasi 2 baada ya kushika Namba 158.

 .

Orodha hiyo ni;

  1. Argentina
  2. Brazil
  3. Germany
  4. Chile
  5. Belgium
  6. France
  7. Colombia
  8. Portugal
  9. Uruguay
  10. Spain
  11. Switzerland
  12. Wales
  13. England
  14. Poland
  15. Italy
  16. Croatia
  17. Mexico
  18. Peru
  19. Costa Rica
  20. Iceland

Kwa upande wa Afrika Uganda bado wanaendelea kuongoza kwa Afrika Mashiriki wakiwa nafasi ya 17 kwa Afrika na 75 duniani wakifuatiwa na Kenya waliopo nafasi ya 20 Afrika na 87 duniani wakati Rwanda wako nafasi ya 27 Afrika na 100 duniani na Burundi nafasi ya 40 Afrika na 138 duniani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *