Mchezaji kikapu wa Pelicans, Anthony Davis ameweka rekodi ya kufunga pointi 52 na kuisaidia timu yake ya upande wa Magharibi kupata ushindi wa pointi 192 kwa 182 dhidi ya timu ya Mashariki.
Kabla ya mechi hiyo ya NBA, maarufu kama All-Star Game Davis amesema kuwa alipania kushinda tuzo ya mchezaji bora wa mchezo huo, maarufu kama MVP.
Nyota huyo wa Pelicans amefanikiwa kuvunja rekodi ya ufungaji ya mchezo huo ya pointi 42 iliyowekwa na Wilt Chamberlain mwaka 1962.
Mchezo wa NBA All-Stars huchezwa kila mwaka kati ya sehemu ya Magharibi na sehemu ya Mashariki mwa nchini Marekani na mwaka huu, mchezo huo ulichezwa katika Uwanja wa Smoothie King ambao ni uwanja wa nyumbani wa timu ya Pelicans.
Mchezo huo pia uliudhuriwa na mwanamitindo wa Tanzania, Jakate Mwegelo ambapo alikutana na Jay Z na Beyonce.