Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Anjella kutoka Konde Gang amesema kuwa, mbunifu wake amesikia maoni na ushauri wa mashabiki wake kuhusu muonekano wake wa kimavazi hivyo anavifanyia kazi.

Akichezesha taya, Anjella ambaye mpaka sasa bado anafanya poa na ngoma yake ya No body anasema kuwa, siyo vibaya kwa mashabiki kumpongeza na kutoa maoni yao pale wanapoona anakosea kwa sababu ndiyo njia sahihi ya yeye kujifunza na kujirekebisha.

“Huwa sikatai watu kutoa maoni juu yangu, tena ndiyo napenda. Baadhi ya mashabiki wangu wamekuwa wakiongelea sana suala la mavazi yangu kuwa siyo mazuri.

Pia amesema kuwa anaomba niwaambie tu kwamba mbunifu wangu (designer) analifanyia kazi,” anasema Anjella ambaye yupo chini ya Lebo ya Konde Gang ya Harmonize.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *