Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Anjella amefunguka na kusema kuwa alitaka kunywa sumu na kutoroka nyumbani wakati anaanza muziki kwasababu mama yake hakutaka mwanae afanye muziki.
Anjella amesema mama yake sio mtu ambaye anapenda muziki kwa sababu ni mtu wa kanisani lakini anamshukuru Mungu amesimamia malengo yake mpaka leo amefanikiwa kusainiwa Konde Gang.
“Nilimwambia mama watanikataza, watanipiga lakini msimamo wangu upo palepale kwa sababu sioni mafanikio yangu mengine nje ya muziki, kuna wakati nilitamani ninywe sumu na kutoroka nyumbani lakini nilituliza akili na kufuata mafundisho ya kanisani ambayo yalinisaidia” amesema Anjella
Wiki iliyopita alifanyiwa party maalum ya kukaribishwa kwenye lebo hiyo ya Konde Gan na tayari ameshaachia kazi yake mpya inayoitwa kama aliyomshirikisha Harmonize.