Angella amewasilisha malalamiko Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), akidai lebo ya Konde Music World Wide inayomilikiwa na Harmonize iachane naye rasmi.

Angella anadai kupewa barua rasmi ya kuachana naye na kumrudishia digital platform zake na kwamba Novemba Mosi, mwaka huu Harmonize alitakiwa afike Basata kwa ajili ya kusikiliza shauri hilo, lakini hakutokea.

“Mkataba ulikuwa unasema Angella akiuvunja atawalipa shilingi bilioni moja, lakini wakiuvunja wao watamrudishia ‘digital platform’ zake tu bila hata senti tano, sasa wanachokifanya ni uhuni, wameachana naye kimtindo ila hawataki kumalizana naye kila mmoja ashike njia yake.

“Kama ni fedha za nyimbo zake na lolote likitokea wanaendelea kunufaika wao na si Anjella ambaye wamemuweka kando,” kilisema chanzo hicho cha kuaminika.

Mbali na hilo, inadaiwa kuwa msanii huyo aliahidiwa na Harmonize kusaidiwa matibabu ya mguu jambo ambalo halikufanyika, huku ikielezwa kuwa sababu za Harmonize kutaka kuachana na nae ni pamoja na kutorudisha faida ya kile walichowekeza kwake

Ikumbukwe hivi karibuni Cheed na Killy nao waliachana na lebo hiyo kisha kumburuta Harmonize BASATA

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *