Muigizaji nyota nchini Marekani, Angelina Jolie amesema kuwa ana wakati mgumu tangu alipoachana na mpenzi wake Brad Pitt mwaka jana.
Jolie amesema kuwa amekuwa na wakati mgumu sana mpaka kukosa furaha kutokana na kutengana kwao na mpenzi wake huyo ambaye pia ni muigizaji wa filamu nchini Marekani.
Lakini najaribu kukabiliana na tatizo hili kwa kuzingatia mambo yajayo na kutambua kwamba ni mambo ya kawaida kwa mwanadamu.
Muigizaji huyo alibadili kazi yake na kuwa muelekezi wa filamu kwa kuzugumzia kuhusu filamu ya First They Killed My Father, filamu hiyo iliotugwa kulingana na hali ilivyokuwa ,itaonyeshwa rasmi kwa mara ya kwanza kwenye mtandao wa Netflix mwezi huu.
Filamu hiyo ilibuniwa mwaka wa 1970 huko Cambodia, na inazungumzia mwanaharakati na mwalimu Loung Ung aliyeepuka chini ya kiongozi wa Pol POT, Khmer Rouge
Pia Jolie amesema ataigiza kwanza , kwa sababu hakuwa na filamu ya kuelekeza aipendayo kama filamu yake ya hivi karibuni.
Jolie amesema jukumu lake la kwanza baada ya mapumziko ”pengine” ni kurekodi filamu yake ya mwaka wa 2014 ya Maleficient.
First They Killed My Father itazinduliwa wikendi hii katika tamasha ya filamu la Telluride huko Colorado.
Maoni kadhaa ya filamu hiyo yameanza kutolewa , miongoni mwao yakiwa mazuri kutoka kwa ripota wa Hollyhood , Scott Feinberg.
Jolie ,amesema filamu hiyo ilitungwa vyema kuhusiana na mapenzi na itawaelimisha watu kuhusiana na historia kali ya Cambodia mwaka 1970.”