Aliyekuwa Mbunge wa Kinondoni (CUF), Maulid Mtulia amekabidhiwa rasmi kadi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) mapema leo katika ofisi za chama hicho.

Mbunge huyo amekabidhiwa kadi leo baada ya kutangaza kujiuzuru nafasi yake ubunge wiki iliyopita.

Katika kujivua kwake mbunge huyo amesema kuwa amejivua nyadhifa zake zote ya Ubunge wa Kinondoni na vyeo vyote alivyokuwa navyo CUF na kuamua kujiunga na CCM kutokana na kuridhishwa na CCM ya sasa na utendaji wa Rais Dk. Magufuli.

Wakati akikabidhiwa kadi hiyo Mbunge huyo amesema kuwa ametoka kwenye chama chenye migogoro mingi na amekuja kwenye chama chenye amani, haki na Demokrasia ya kweli.

Pia amesema kuwa “Sijaja CCM kutafuta cheo bali nimetumia haki yangu ya kidemokrasia ya kujiunga na chama chochote kile ninachokitaka. Kila jambo nililokuwa namwomba Rais tena hadharani (mfano wakati wa ufunguzi wa maghorofa) ameyatekeleza kwa kiwango kikubwa.

Amesema kuwa “Nawashangaa Viongozi wa Upinzani wanaopinga na kususa mambo ya Serikali na shughuli za Bunge, hizo shida za Wananchi Nani atawatatulia endapo wanawasusia wenye mamlaka? Nipo tayari kuwa hata Balozi wa nyumba kumi na ikishindikana nitaenda kuvua samaki nyumbani Rufiji.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *