Aliyekuwa makamu wa rais wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa amemtaka Rais Robert Mugabe ajiuzulu mara moja ili nchi hiyo iwe salama.

Emmerson Mnangagwa amesema alitoroka nje ya nchi wiki mbili zilizopita wakati alipobaini kuwa kuna njama za kumuua na hatarejea nchini hadi atakapohakikishiwa usalama wake.

Chama cha rais wa Zimbabwe Robert Mugabe kinatarajiwa kuanza mchakato wa kupiga kura ya kutokuwa na imani nae.

Afisa wa Zanu-PF amesema kuwa hoja ya kumnyang’anya urais itawasilishwa bungeni leo Jumanne na mchakato wa kumg’oa madarakani unaweza kuchukua siku mbili tu.

Mashtaka yaliyomo kwenye hoja hiyo ni pamoja na kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 93 “kumpa madaraka makubwa ya kikatiba mkewe Grace, na kushindwa kuheshimu katiba”.

Viongozi wa kijeshi , ambao wiki iliyopita waliingilia kati kuchukua mamlaka ya nchi walisema atakutana na makamu wake wa rais wa zamani aliyeuhamishoni karibuni.

Mugabe ”alimwachia mkewe mamlaka ya kikatiba, licha ya shinikizo kubwa Bwana Mugabe aliwashangaza wengi kwa kukataa kujiuzulu, na badala yake katika hotuma yake kupitia televisheni alisema kuwa ataongoza mkutano mkuu wa chama Zanu-PF.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *