Aliyekuwa Makamo wa rais Zimbabwe Emerson Mnangagwa atangazwa kuwa Rais mpya wa chama cha ZANU-FP.
Mapema leo ametua uwanja wa ndege wa jeshi wa ManyameAkaunti ya chama cha Zanu PF inasemama kuwa Emmerson Mnangagwa amefanywa kuwa rais wa mpito.
Mnangawa mwenye umri wa miaka 75 alifutwa kama makamuu wa rais kutokana na kile serikali ilisema kuwa kutokuwa mtiifu.
Kufutwa kwake kulionekana kama nia ya kumwezesha mke wa Rais Mugabe, Grace, kufuata nyayo za mumewe na kuwa kiongozi wa Zimbabwe.
Bw. Mnangagwa ambaye ni mku wa zamani wa ujasusi amekuwa mtu ambaye alitarajiwa kumrithi Rais Mugabe 93.
Kufutwa kwake kulimaanisha kuwa Grace Mugabe anatarajiwa kuteuliwa kuwa makamu wa rais wakati wa mkutano maalum wa chama tawala cha Zanu-PF mwezi ujao.
Wakati huo huo jeshi linamshikilia waziri wa fedha Ignatius Chombo, Waziri wa Elimu Prof. Jonahan Moyo Afisa Mwandamizi ndani ya chama cha ZANU-PF Savior Kasukuwere.