Aliyekuwa mlinzi wa maslahi ya umma nchini Afrika Kusini, Thuli Madonsela amefanikiwa kushinda tuzo ya mtu mashuhuri zaidi wa Forbes wa mwaka 2016.

Madonsela aliwashinda marais watatu wa Afrika, raia mwenzake wa Afrika Kusini na watu wan chi ya Rwanda katika kushinda tuzo hiyo.

Rais John Pombe Magufuli na mwenzake Ameenah Gurib wa Mauritania walikuwa wameteuliwa kushindania tuzo hiyo.

Mwingine ni mfanyabiashara wa Afrika Kusini Michiel le Roux ambaye ni mwanzilishi wa benki ya Capitec.

Madonsela, aliyetangazwa mshindi kwenye hafla iliyoandaliwa Nairobi jana jioni amejulikana kwa msimamo wake mkali dhidi ya ufisadi alipokuwa anahudumu kama mlinzi wa maslahi ya umma Afrika Kusini.

Alihudumu kuanzia mwaka 2009 hadi 14 Oktoba mwaka huu, muhula wa miaka sita.

Kipindi hicho, alimchunguza rais, akawachunguza wakuu wa polisi, maafisa wakuu serikalini na hata wanasiasa wa upinzani.

Uchunguzi wake ulipelekea kusimamishwa kazi kwa mkuu wa polisi Bheki Cele mwaka 2011.

Aliwahi kumchunguza pia kiongozi wa chama cha upinzani cha Economic Freedom Fighters Julius Malema ambaye mwishoni mwa kipindi chake, alimuunga mkono alipofanya uchunguzi kuhusu uhusiano wa Rais Jacob Zuma na familia tajiri ya Gupta.

Pia alimchunguza pia Rais wa sasa wa Afrika Kusini Jocb Zuma kuhusu ukarabati uliofanyiwa makao yake Nkandla.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *