Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Alikiba yupo nchini Marekani kwenye tour yake ya album yake ya Only One King ambayo ataifanyia katika miji 10 nchini humo.
Katika tour yake hiyo Alikiba amekutana na mwanaharakati wa mitandaoni Mange Kimambi tena wakiwa wote na kupiga picha pamoja, sio kupiga picha tu hata kucheza pamoja.
Wakiwa katika picha ya Pamoja Alikiba na Mange Kimambi wameonekana wakicheza Pamoja na kukata keki nchini Marekani.
Alikiba amekuwa na uhusiano mzuri na Mange Kimambi japokuwa wakati mwingine wanakwazana kutokana na tabia za Mange Kimambi.