Wanamuziki wa Bongo Fleva, Alikiba na Shilole wamemaliza tofauti zao baada ya wawili hao kupanda jukwaa moja na kutoa burudani mkoani Kigoma.

Alikiba na Shilole walikuwa na tofauti na kurushiana maneno kwenye interview na mitandaoni kuhusu mualiko kwenye uzinduzi wa Album ya Alikiba ‘The Only One King’.

Wawili hao wamekubali kumaliza tofauti zao baada ya Alikiba kumpandisha kwenye stage Shilole kuimba na kucheza pamoja.

Kwenye video Shilole anaseema Tunaishi kwa kusapotiana, Alikiba namkubali, ila twende tukawatoe watu utata ulisema hukunialika na Alikiba alikubali kwamba amemualika“.

Alikiba alikuwa na onesho lake mkoani Kigoma ambapo mashabiki wake walijitokeza kwa wingi kwa ajili ya kupata burudani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *