Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Alikiba ameamua kutumia nguvu yake ya ushawishi katika tasnia kwa kufanya kazi na baadhi ya wasanii wa ndani, tofauti na mastaa wengi wakubwa kwa lengo la kusukumu muziki wao mbele.

Staa huyo akitoa shavu kwa wasanii mwaka huu hajatoa wimbo wowote mpya tangu Oktoba 4, 2021 alipoachia albamu yake ya tatu, ‘Only One King’ yenye nyimbo 16 alizoshirikisha wasanii kutoka nchi tano tofauti.

Kwa wengine wanatazama mpango huo kama kulipa deni baada ya albamu yake, ‘Only One King’ kuwashirikisha wasanii wa Bongofleva walio chini ya lebo yake pekee ambao ni Abdukiba, K2ga na Tommy Flavour.

Mpango huo unatarajiwa kumuondoa Alikiba katika lawama kuwa wasanii wakubwa wenye rekodi lebo Bongo wamekuwa wabinafsi kwa kupendelea kufanya kazi na wasanii walio chini ya lebo zao pekee.

Meneja wa Alikiba na Kings Music kwa ujumla, Aidan anasema kuwa huo sio mpango wa menejimenti, bali ni uamuzi wa Kiba kuwapa shavu wasanii wenzake.

Anasema wasanii wengi wanapenda kufanya kazi na Kiba, ila kuna wakati anakuwa na ratiba ngumu inayombana, wakati huu amepata nafasi ndiyo maana amefanya nao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *