Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Alikiba amefunguka Kuhusu Kutoa Album ambapo amesema kuwa ipo Katika hatua za mwisho kabisa na kusema itatoka Hivi Karibuni.

Alikiba amesema kuwa Album yake mpya ipo kwenye final stage itatoka hivi karibuni hivyo amewataka mashabiki wake kuingojea hiyo albam baada ya kukamilika tayari na mashabiki wataipata albam hiyo.

Kuhusu kutoa nyimbo za kulalamika Alikiba amesema kuwa hawezi kumfurahisha kila mtu! Ngoma za kuchezeka anazo huwa anafanya muziki kulingana na season kwani December zimetoka ngoma nyingi za kuchezeka.

Kuhusu kuimba kifaransa kwenye wimbo wa Infidele Alikiba amesema kuwa kiukweli mimi sio mfaransa ila nimejifunza, nilichoimba kwenye kipande cha kifaransa ni kama marudio tu ya verse ya kwanza ila imebadilika lugha tu, lakini ujumbe ni ule ule.

Amesema kuwa ”Nilifikiria tu kuwa jamii ya watu wengi duniani wanaongea kifaransa hivyo nikaona ni jambo zuri, japo kwenye matamshi ilikuwa kazi kubwa sana na nitoe shukrani kwa msichana mmoja anaitwa Aaliyah, wakati nikiwa Afrika Kusini naandika huu wimbo alinisaidia sana

Pia alikiba amezungumzia mahusiano kwa kusema kuwa Kwenye mahusiano amewahi kusalitiwa sana, sisi ni binadamu hatujakamilika na mara nyingi watu wanatumia mapungufu yetu kutuumiza! Ndio maana inakuwa Infidele”.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *