Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Alikiba amefunguka kuwa Team Kiba hawatakubali tena kufungwa na Team Samatta katika mechi ya hisani ya SamaKiba Foundation ambao unakwenda kupigwa Uwanja wa Taifa Dar, Agosti 8, mwaka huu.
Kiba amesema walikuwa na bahati mbaya katika misimu miwili iliyopita na kujikuta wakifungwa katika mechi zote mbili, licha ya kuwa kikosi chao kilikuwa bora zaidi ya kile cha Team Samatta, hivyo awamu hii ni ni zamu yao kuwapa raha mashabiki wa TeamKiba.
Mchezo huo wa SamaKiba Foundation ulianzishwa kwa kuunganisha nguvu kati ya nahodha wa Taifa Stars na nyota wa Aston Villa ya England, Mbwana Samatta na msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Alikiba kwa lengo la kukusanya fedha na kuzisaidia jamii za watu wa hali ya chini.
Mbwana Samatta tayari ameshatangaza timu ya watu watano ambao ni Mohamed Samatta, Idd Seleman ‘Nado’, Farid Mussa na Juma Kaseja na msemaji wake ni Haji Manara, ambaye ni Ofi sa Habari wa klabu ya Simba.
Huku wasanii wake wawili wa Kings Music, K2ga na mdogo wake Abdu Kiba wakitajwa kuwa sehemu ya kikosi hicho.
Matokeo yaliyopita yalikuwa hivi, msimu wa kwanza ambao ulikuwa ni Juni Mosi, 2018, Team Samatta 3-1 TeamKiba, huku msimu wa pili uliofanyika Juni 11 mwaka jana, Team Kiba walifungwa 6-3.