Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Alikiba amepokea tuzo zake rasmi kutoka YouTube kutokana na nyimbo zake kufanya vizuri katika mtandao huo.
Alikiba amepokea tuzo hizo mbili kwa pamoja, ya kwanza ni ya kufikisha Subscribers laki moja (100,000) na nyingine ya kufikisha Subscribers Milioni Moja (1,000,000).
Akaunti hiyo ya YouTube ya Alikiba aliaacha kuitumia kwa muda wa zaidi ya miaka miwili kwa kile kinachosemekana kukatisha mkataba na kampuni ya Sony Music.
Kutokana na hayo Alikiba alilazimika kutumia akaunti ya YouTube ya Kings Music kabla ya kurejeshewa akaunti yake hiyo kutokana na makubaliano yao.