Staa wa Bongo Fleva, Alikiba jana alimtembelea mama mzazi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli nyumbani kwake Chato mkoani Geita.

Kiba aliongozana na mdogo wake Abdukiba ambaye pia ni msanii pamoja na wadau wake kufika wilayani humo.

Kabla ya kufika nyumbani hapo, Kiba na timu yake walianza kutembelea hospitali ya wilaya ya Chato kwa ajili ya kuwafariji wagonja waliolazwa hospitalini hapo pamoja na kutoa misaada kwa wagonjwa.

Kupitia akaunti yake ya Instagram Alikiba ameandika

 “leo tuliweza kutembelea HOSPITAL ya wilaya Ya CHATO Kwenda Kuwaona Wagonjwa Na vile vile tulikwenda Nyumbani Kwa muheshimiwa RAISI natuliweza kupiga Story Na BIBI yetu MAMA JPM .Nimcheshi Sana na tulipata baraka zake,“.

Alikiba alikuwa wilayani Chato kwa ajili ya show yake ya fungua mwaka na Kiba iliyofanyika jana Chato mkoani Geita.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *