Mwanamitindo wa Bongo, Jokate Mwegelo amesainiwa chini ya lebo ya Alikiba inayotarajia kuanza kazi hivi karibuni.
Hayo yamesemwa na msanii mkongwe wa Bongo Fleva, Abby Skills ambaye pia yupo chini ya lebo hiyo.
Amesema kuwa “Mimi pia nipo chini ya lebo yake, Alikiba ni bosi wangu, kuna Abdu Kiba, kuna Salim, kuna Heri, kuna Jojo Jokate”,.
Alikiba na Jokate waliwahi kuwa na tetesi kuwa na mahusiano ya kimapenzi, na hivi karibuni Alikiba alisikika akisema hadharani kwamba hana mahusiano na mwanamitindo huyo.
Alikiba anatarajia kutambulisha lebo yake hiyo itakayokwenda kwa jina la King Music ambayo itakuwa ina manage wasanii kama ilivyokuwa WCB.