Mwanamuziki nyota wa Bongo Fleva, Alikiba amesema kuwa anatarajia kuachia albam kabla ya kumalizika kwa mwaka huu ambayo itakuwa na wasanii tofauti wa kimataifa.
Alikiba ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya kwasili nchini akitokea Afrika Kusini alipokwenda kwa ajili ya ziara yake ya kimuziki nchini humo.
Mwanamuziki huyo ambaye kwasasa anatamba na wimbo wake ‘Aje remix’ amesema kuwa albam hiyo itakuwa na nyimbo za kutosha ambapo amewashirikisha wasanii tofauti wakiwemo wa nje ya nchi na ndani ya nchi.
Pia aliakiba ameawashukuru mashabiki wake waliojitokeza kwenda kumpokea uwanja wa ndege alipokuwa anawasili kutokea Afrika Kusini ambapo alikabidhiwa tuzo yake ya mwanamuziki bora wa Afrika MTVEMA.
Alikiba kwasasa yupo nchini Marekani kwa ajili ya ziara yake ya kimuziki nchini humo katika mjini mitano kabla ya kuelekea bara la Ulaya.