Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Alikiba amekanusha taarifa zilizosambaa katika mitandao ya kijamii kuwa mke wake Amina anaujauzito.

Alikiba amesema kuwa taarifa hizo siyo za kweli kwasababu hana ujauzito ila watu wameamua kusambaza habari hizo kwenye mitandao ya kijamii.

Kiba amesema kuwa tangu amefunga ndoa amebadili tabia yake na kwasasa anamuheshimu sana mke wake lakini pia usumbufu wa wanawake kumtongoza mitandaoni  umepungua sana kwa kuwa wanajua kaoa.

Mwanamuziki huyo ameongeza kwa kusema kuwa kwasasa amekuwa akijiheshimu na kumuheshimu mke wake tofauti na alivyokuwa kipindi hajaoa ambapo wasichana walikuwa wakimsumbua.

Pia Kiba alimalizia kwa kusema kwamba haongozani na mke wake mara kwa mara kwa kuwa mke wake ni msomi ambaye yupo ‘busy’ na kazi zake, lakini pia mke wake sio mtu wa kupenda kuonekana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *