Mwanamuziki nyota wa Bongo Fleva, Alikiba amewamba radhi mashabiki zake baada ya kushindwa kufanya show wiliyani Chato mkoani Geita.
Alikiba alitakiwa kufanya show katika mji wa Chato Mkoani Geita na kudai kuwa alishikwa na homa kali na kushindwa kuhudhuria katika show hiyo.
Baada ya Alikiba kukosa show hiyo lakini mdogo wake Abdukiba alifanya show ya kufa mtu na kuwakosha mashabiki waliotokeza kwenye ‘party’ hiyo.
Kupitia akaunti yake ya Instagram Alikiba ameandika ” Juzi nilitakiwa kujiunga na mashabiki wangu wa chato Geita, nyumbani kwa Baba yetu Muheshimiwa Rais lakini nilishikwa na homa kali ila leo naendelea Vizuri samahani kwa kutokuwepo lakini nawaahidi nitarudi tena kwa nguvu zote Mungu akipenda hivi karibuni tutawaandalia show ya kipekee lakini vilevile Abdukibaa mdogo Wangu aliniwakilisha vema namshukuru sana “.
Pia Alikiba amedai kuwa hali yake kiafya sasa iko poa kwani anaendelea vyema na kudai wanajipanga kuona jinsi gani wanaweza kufungua mwaka vizuri 2018 kutokana na kuugua kwake kuharibu mipango yake ikiwa pamoja na kushindwa kufanyika kwa funga mwaka na Alikiba.