Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Alikiba amefunga ndoa na mpenzi wake Aminah Rikesh leo asubuhi jijini Mombasa nchini Kenya.
AliKiba amefunga ndoa hiyo katika msikiti wa Ummul Kulthum jijini Mombasa ambapi ndoa hiyo imefungwa na Sheikh Mohamed Kagera.
Sherehe itafanyika hapo baadae na inatarajiwa kuhudhuriwa na watu maarufu kutoka maeneo mbalimbali.
Alikiba ameungana na wasanii wenzake wa Bongo Fleva waliofunga ndoa kama vile AY, Mwana FA, Tunda Man pamoja na Dogo Janja.