Muigizaji wa Bongo Movie, Irene Uwoya amedai kwamba watu wengi katika karne hii ya sasa wanateseka na mapenzi na hivyo akawataka wote walioshindwa na mapenzi basi wajaribu bahati yao katika kilimo, pengine huko ndiko bahati yao ipo.

Uwoya amedai kuwa, haina haja mtu kujiingiza kwenye mapenzi wakati matokeo yake ni maumivu kutwa kucha, wakati furaha yako iko kwenye kilimo huku akiongeza kuwa atakayefuata ushauri wake basi atamshukuru mbeleni.

Maneno hayo ya Uwoya yalipokelewa kwa mitazamo tofauti huku baadhi wakisema kwamba kuna waliojaribu vyote na tayari wameshindwa na kutaka ushauri zaidi kupewa jaribio la fani ya tatu mbali na kilimo na mapenzi.

Muigizaji huyo mkongwe ambaye pia ni mama wa mtoto mmoja, baadhi ya mashabiki walitumia kigezo hiki kumuuliza kwa kuwa yeye ametendwa sana katika mapenzi ana mashamba mangapi iwapo aliamua kujaribu kilimo.

“Una mashamba mangapi mpaka sasa? Maana wewe ni mfano hai wa waliokucheka kwenye mapenzi,” mwingine alitoa maoni.

Uwoya katika siku za hivi karibuni ameonekana kutolea ushauri komavu kwa mashabiki zake tangu miezi michache iliyopita.

Hivi karibuni alialikwa kwenye sherehe ya kanisa kama mgeni maalum katika ibada ya kusherehekea miaka minane tangu kanisa hilo lililopo mjini Morogoro kuanza kutoa huduma ya uponyaji na mahubiri.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *