Waziri wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Mkuchika amesema kuwa ataanza kuhakikisha watumishi wa Umma wanatumia muda wao kufanya kazi kwa ajili ya watanzania.
Waziri Mkuchika ambaye leo ameapishwa na Rais Magufuli kuwa Waziri wa wizara hiyo amesema kuwa katika kipindi chake atahakikisha wafanyakazi wanalipwa mshahara kulingana na kazi zao na wanatumia muda wa kazi kufanya kazi za serikali.
Pia Mkuchika amesema kuwa kwa sasa watumishi wengi wa Umma wanalipwa mshahara kamili kwa kufanya kazi robo za serikali jambo ambalo yeye atakwenda kulisimamia na kuhakikisha kuwa watumishi hao wanafanya kazi kamili ili walipwe kulingana na kazi zao kamili.
Mbali na hilo Mkuchika amedai kuwa atakwenda kuongea na Waziri wa Elimu ili ikiwezekana somo la Rushwa lianze kufundishwa kuanzia shule ya awali nchini mpaka vyuo vikuu na kusema watu wamekuwa wakichukua na kutoa rushwa kwa kuwa hawana elimu ya kutosha juu ya athari ya rushwa.