Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Aslay amesema kuwa alikuwa na wasiwasi mkubwa kufanya kazi peke yake bila ya Meneja wake Mkubwa Fella.
Aslay amesama kuwa kutokana na woga na wasiwasi huo ndipo hapo alipoamua kumtafuta meneja wake wa sasa Chambuso na kuanza kufanya kazi pamoja.
Amesema kuwa “Nilikuwa na wasiwasi mkubwa sana kwamba tunaweza kusonga bila Mkubwa nyuma au Menenjimenti yoyote baada ya hapo nikamtafuta Chambuso na yeye akaniambia kuwa tunaweza kusonga mbele.
Pia ameendelea kusema kuwa tukaanza kazi nakumbuka kazi yangu ya kwanza ilikuwa inaitwa ‘Angekuona’ hiyo niliachia kwenye TV na Radio mbalimbali, huo ndiyo wimbo ambao mimi unanigusa kutoka moyoni kwa sababu ni maisha yangu halisi kabisa”.
Hata hivyo, Aslay amesema kwa sasa bado hajapata mafanikio makubwa ila anaamini kuwa atapata mafanikio makubwa mbeleni na baadaye kuja kuwa kama wasanii wengine wakubwa ambao wananufaika vizuri kupitia muziki wao.