Aliyekuwa mke wa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Ben Pol aitwae Anerlisa Muigai amefunguka na kusema kuwa kuna ex-wake alitaka amfungulie biashara, jambo ambalo alilikataa na huo ukawa mwisho wa penzi lao.
Mrembo anasema kuwa, suala la kuomba pesa kila wakati katika mapenzi ni kitu ambacho alikuja kubaini kuwa watu wanaenda kwake kwa ajili kujinufaisha na siyo mapenzi.
“Nilikuwa kwenye mahusiano ambapo mwenzi wangu alianza kuniambia nimwambie pin ya ATM, wakati mwingine nikiongea na mama yangu anataka kujihusisha na mazungumzo yetu.
“Wacha nicheke, mmoja wa ma-ex wangu aliniuliza tumekuwa pamoja kwa mwaka mmoja kwa nini nisimsaidie kama vile kumjengea nyumba na hata kumfungulia kampuni kama yangu, nilimjibu nikamwambia kama uliona kuanzisha uhusiano na mimi kutakutajirisha haya basi uko kwenye uhusiano ambao haufai,” anasema Anerlisa.
Anerlisa aliwahi kuolewa na Ben Pol, lakini ndoa yao ikadumu kwa muda mfupi. Katika