Mbunge wa Kigoma mjini kwa tiketi ya ACT Wazalendo amefunguka na kuwataka watu wasirudishwe nyuma kwa vitisho na usumbufu wa sheria kandamizi zinazopelekea baadhi ya viongozi kukamatwa na kuwekwa ndani.

Zitto Kabwe ameweka wazi hayo mara baada ya kuachiwa leo Februari 23, 2018 na kusema kuwa yeye anaendelea na harakati zake ya kuwafikia viongozi na Kata ambazo wananchi waliwachagua viongozi wa ACT Wazalendo.

Zitto Kabwe ameonyesha kuguswa na muaji mengine ambayo yametokea jana ambapo diwani wa CHADEMA ameauwa kwa kukatwa mapanga sehemu mbalimbali katika mwili wake

Pia amesema kuwa “Nawapa pole Wananchi wa Ifakara kwa msiba wa Diwani wao aliyekatwa mapanga mpaka kufa jana Usiku. Nilipata taarifa hizo nikiwa selo ya Polisi. Mauaji ya namna hii kwa Viongozi wa kisiasa yanatia doa nchi yetu na ni mwendelezo ya uvunjifu mkubwa wa haki za raia”.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *