Waziri wa Habari, utamaduni, sanaa na micheo Dr. Harrison Mwakyembe amesema kuwa hawezi kuifanyia kazi ripoti ya Nape kuhusu mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuvamia kituo cha Clouds Media kutokana na ripoti hiyo kutokamilika.
Mwakyembe amesema kuwa yeye kama mwanasheria ni mwiko na hatopeleka taarifa ambayo haijakamilika kwa wakubwa wake.
Waziri huyo amesema kuwa huwezi kuwa Hakimu kwenye suala lako wewe mwenyewe, kufanya hivyo ni ubatili kwahiyo hata mimi ningekuwa ni mwandishi wa habari ningesema hili jambo siliwezi kwakuwa linanihusu na mimi.
‘Kanuni zinataka kusikiliza upande wa pili, sasa mmeshasema kitu kina upande mmoja alafu nimpelekee kiongozi wangu, mimi kazi yangu ni kupata maelezo ya upande wa pili na nitapata’.
‘Hili jambo ni lakufa na kupona, yani niache kukutana na wakuu wa idara mbalimbali hapa kuhakikisha nakuza suala la sanaa na kuhakikisha vijana wetu hawaendelei kuibiwa nibaki kuhangaikia suala la ripoti’ .
‘Mimi sikuapa kwa jambo hilo moja pekee lakini mimi ni mwanasheria mkongwe na nitahakikisha nalifuatilia lakini mimi sitaunda kamati katika jambo hilo’ .
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda anashtumiwa kuvamia ofisi za Clouds Media zilizopo maeneo ya Mikocheni B jijini Dar es Salaam akiwa na askali wenye silaha kali.