Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho amepongeza kazi nzuri iliyofanywa na wachezaji wake ya kupambana na kufanikiwa kupata bao la ugenini katika mchezo wa mzunguko wa kwanza wa hatua ya 16 bora wa Europa League dhidi ya FC Rostov ya Urusi.

Kiungo mshambuliaji kutoka Armenia Henrikh Mkhitaryan alifunga bao la Man Utd katika dakika 35, kabla Aleksandr Bukharov hajaisawazishia Rostov dakika ya 53.

Jose Mourinho amewaambia waandishi wa habari kuwa, kikosi chake kilicheza vizuri na imekua faraja kwa kila mmoja wao kuondoka katika uwanja wa ugenini wakiwa na matokeo ya sare.

Mourinho amesema inapendeza kuwa na bao la ugenini, ambalo ana imani litawasaidia katika mchezo wa mkondo wa pili ambao utachezwa juma lijalo kwenye uwanja wa Old Trafford.

Katika mchezo huo, Man Utd watatakiwa kusaka ushindi na ikishindikana watalazimika kutafuta angalau matokeo ya bila kufungana ili kufanikisha safari ya kutinga kwenye hatua ya robo fainali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *