Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Harmonize amefunguka kwa mara ya kwanza baada ya kuachana na wasanii wake Killy na Cheed.

Kupitia akaunti yake ya Insta Story Harmonize amesema kwamba anawaamini hawatomuangusha pia wana kila sababu ya kuwa wasanii wakubwa.

Harmonize ameandika kwamba “My brother Killy na Cheed, mna kila sababu ya kuwa wasanii wakubwa katika hili Taifa bila shaka nji ni nyeupe nawaaminia sana”. 

“Nina imani hamtoniangusha, video 2 zilizopo ndani kwa gharama ya Management zilizoongozwa na Travellah zikawe mwanzo wenu mwingine mwema”. 

Killy na Cheed wamedumu kwa miaka miwili Kondegang tangu wakitokea lebo ya Kings Music ya Alikiba.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *