Mkali wa Hip Hop Bongo, Billnass amesema kuwa hakwenda kituo cha polisi kuwaangalia mabosi zake waliokuwa wametuhumiwa kujishughulisha na dawa ya kulevya ili wajifunze maisha.

Billnass anayetamba na ngoma yake ‘Mazoea’ amesema katika maisha aliyoishi yeye suala la kwenda ndani ni jambo la kawaida sana hivyo kutokwenda kuwaona maboss zake ambao ni Pet Man na Mchafu Chakoma kipindi wamepatwa na matatizo si jambo la msingi.

Mwanamuziki huyo amesea kuwa hawezi kuhama label yake ya (LFLG) kwa ajili ya maboss zake wamehusishwa na dawa za kulevya.

Kwa upande mwingine Billnass ameongeza kuwa Mwana FA kumfunika katika wimbo wake wa Mazoea aliomshirikisha ni heshima sana kwakwe kwa kuwa msanii huyo ni mkongwe kwenye muziki.

Pia msanii huyo amekanusha kuwahi kuwa na mahusiano na msanii Linnah Sanga ambaye ukaribu wao ulifanya watu wengi kuhisi kwamba ni wapenzi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *