Mkurugenzi wa Kituo cha Radio cha ETV na Radio E, Majizo amemmwagia sifa mke wake Elizabeth Michael baada ya wawili hao kufunga ndoa mwezi uliopita.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Majizo ameanza kwa kuandika Kwanza ni shukrani kwa kila mtu aliyehusika kufanikisha ndoa yangu na mke wangu Eliza. Ndugu, marafiki na jamaa wote asanteni sana.
Ameendelea kwa kusema kuwa Nawashukuru kwa namna mlivyonielewa hasa katika style tuliyochagua kufunga ndoa yetu, imenipa faraja kuona watu wangu wote wamekuwa waelewa na kulipokea positively. Asanteni.
Lakini kipekee sana shukrani zangu ni kwa Mke wangu. Namshukuru kwa namna alivyokuwa muelewa nyakati zote, alikuwa mhanga wa maneno, matusi, kejeli na yote aliyopitia kutokana na mahusiano yetu.
Pia amesema kuwa Aliambiwa ana uchumba sugu, mara pete inakata kidole lakini yote hayo hayajawahi kumtia unyonge wala kumtoa kwenye mstari wa kile tunachoamini sisi. Hajawahi kunipa presha, hajawahi kuonesha dalili za kukosa subra kwa kuwa mimi na yeye tulijua ni nini tunafanya.
Mwisho amemalizia kwa kuandika Naomba spirit hiyo iwe funzo kwa wadogo zangu wanaowaza kuoa au kuolewa, tembeeni kwenye njia yenu, fanyeni mambo kwa wakati mnaotaka ninyi huku MKIMTANGULIZA MUNGU. Msiyumbishwe na maneno ya watu, na Mungu atawasaidia.